26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 21, 2024

Contact us: [email protected]

Watumishi wasimamishwa kazi Dodoma

rebeccaRamadhan Hassan, Dodoma

SERIKALI imewasimamisha kazi maofisa biashara wawili wa Mkoa wa Dodoma kutokana na kuchelewesha utoaji wa leseni za biashara.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka ofisi ya Rais (TAMISEMI), Rebbeca Kwandu, aliwataja waliosimamishwa kazi kuwa ni Elias Kamara na Donatila Vedasto.

“Agizo hili limetolewa na Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene baada ya kupokea malalamiko mengi kutoka kwa wafanyabiashara ambao ilionesha uwapo wa mazingira ya rushwa katika utoaji wa leseni za biashara’’alisema Kwandu.

Alisema maofisa hao, wamesimamishwa kutokana na  uchunguzi uliofanyika katika Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma na kugundua  kulikuwa na maombi ya leseni 750 ambayo hayajashughulikiwa bila ya sababu za msingi.

Alisema hali hiyo, imeifanya manispaa hiyo kupoteza mapato ya Sh milioni 75, jambo ambalo haliwezi kuvumiliwa.

Alisema tayari Simbachawene, ametoa maagizo kwa mkurugenzi wa manispaa hiyo kujaza nafasi hizo kwa kukaimisha watu wenye sifa.

Alisema pia waziri ameagiza mamlaka za Serikali kuhakikisha zinatoa leseni za biashara bila urasimu wowote.

“Nawaomba wanaohusika kutoa  leseni kwa wahusika na wapatiwe  ndani ya siku mbili au tatu pamoja na kuacha urasimu ili kujiepusha na vitendo vya rushwa,’’ alisema Kwandu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles