Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Watumishi wanawake kutoka Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) wameungana na Wizara na sekta binasi pamoja Taasisi nyingine nchini kuadhimisha kilele cha maadhimisho ya Siku ya wanawake Duniani kilichofanyika katika Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma tarehe 8Machi2023.
Maadhimisho hayo yaliongozwa na kauli mbiu isemayo Ubunifu na mabadiliko ya teknolojia chachu katika kuleta usawa wa kijinsia, ambapo Mgeni rasmi wa maadhimisho hayo alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule.
Akizungumza katika maadhimisho hayo Machi 8, mwaka huu, Senyamule alisesema lengo la kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ni kutaka kuhamasisha jamii juu ya uwezo wa wanawake katika kuleta Usawa wa Kijinsia na maendeleo ya kiuchumi, na kuisistiza kuwepo kwa usawa wa kijinsia mahala pa kazi hususan katika shughuli zote za maendeleo ikiwemo nafasi za maamuzi, siasa na umiliki wa mali pamoja Ardhi.
Aliongeza kuwa wanawake ni Jeshi kubwa wakiwezeshwa wanaweza na wamesisitizwa kuepuka vishawishi vya kuingia kwenye ndoa za jinsia moja.
Mwenyekiti wa TUGHE tawi la TACAIDS, Magreth Mrema akizungumza baada ya maandamano alisema mshikamano kwa wanawake ni jambo la msingi ikiwa ni pamoja na kuwa chachu ya mabadiliko ya tabia kuanzia katika familia ,jamii kwa ujumla.