33.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

Watumishi wa Umma wahimizwa kujikwamua kimaisha na Bayport

*Manara awakumbusha wanamichezo kuchangamkia fursa

Na Faraja Masinde, Mtanzania Digital

Watumishi wa Umma nchini wametakiwa kuchangamkia mikoko inayotolewa na Taasisi ya Bayport ili kujikwamua kimaisha.

Hayo yameelezwa Dar es Salaam leo Jumatano Julai 7, 2022 na Afisa Uendeshaji wa Bayport, Erigo Materu katika hafla ya kuingia mkataba wa Ubalozi na aliyekuwa Afisa Uhamasishaji wa Klabu ya Yanga, Haji Manara.

Materu amesema kuwa baada ya kuwapo sokoni kwa miaka 16 kuna mambo ambayo imejifunza ikiwapo umuhimu wa muda na gharama katika utoaji wa mikopo hatua ambayo imeisukuma kutoa huduma kwa njia ya kidigital.

“Hii ina maana kwamba mtumishi wa umma kwasasa anapohitaji mkopo anaweza kuupata bila hata kuonana na sisi wala kuhitaji makaratasi mengi.

“Tumejifunza umuhimu wa muda na gharama katika maisha ya Mtanzania, hivyo mtumishi anauwezo wa kupiga simu na kupata mkopo papohapo bila kujaza karatasi lolote.

“Lakini pia mtumishi huyu anaweza kuwa nyumbani kwake akabonyeza 15049# akakopa palepale, sasa haya yote tunayafanya ili kurahisisha Watanzania kupata mikopo.

“Hivyo mtumishi anaweza kupiga namba 0800782700 na kwa kuzungumza tu ukapata mkopo, hivyo ndiyo sababu tukaingia mkataba na Haji Manara kwa kuwa tunaamini kuwa ni mfuasi wa mabadiliko na ataweza kulisukuma hili kufika kwa Watanzania walio wenge,” amesema Materu na kuongeza kuwa lengo ni kuhakikisha kuwa maisha ya wengi wanaimarika.

Upande wake Manara mbali na kuishukuru taasisi hiyo amewasihi wachezaji mpira nchini kuhakikisha kuwa wanachangamkia fursa za ubalozi ili waweze kutumia umaarufu wao kujipatia kipato.

“Mimi nimekuwa kwenye tasnia ya mpira wa miguu kwa muda mrefu ambapo zamani tulikua hatupati nafasi hizi, sasa mambo amebadilika.tumebrand mpira wa miguu na ni heshima sana kuona leo tunatambulika na kupewa ubalozi.

“Kama mnavyojua kwamba kwangu sina jambo dogo ingawa kwa wakati mwigine unaweza uniletee tabu, hivyo ujumbe utafika vile ambayo ni zaidi ya matarajio.

“Bayport ipo kwa utaratibu na msingi na nafuata masharti ya Benki Kuu hii ni taasisi ya kifedha ili nifanye kazi lazima nijiridhishe kinachofanyika ni kwa manufaa ya nchi.

“Hii nchi bado waliowengi watumishi wa umma bado ni masikini Serikali inatakiwa kupata uungwaji mkono wa taasisi kama hizi,” amesema Manara na kuongeza kuwa:

“Zamani ilikua na mlolongo mkubwa sasa naomba mkopo kwa namba simu tu mzigo upo pale hauhitaji uonane nao ni simu tu.

“Tulikua kwenye mpira hasa wachezaji wote watu mashuhuri wenye pesa ni watu wa mpira, hivyo wachezaji wetu waamke watumie ukubwa wa majina yao kutengeneza fedha,” amesema Manara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles