Na MOHAMED HAMAD, KITETO
SERIKALI wilayani Kiteto, mkoani Manyara, imewataka wananchi kuacha kuwatishia watumishi wa Serikali kwa imani za kishirikina, hali inayowafanya waogope na kukimbia makazi yao.
Akizungumza katika ya Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto hivi karibuni, Ofisa Utumishi wa Wilaya ya Kiteto, Raphael Makoninda, alisema japo Serikali haiamini uchawi lakini imekuwa tishio kwa baadhi ya watumishi wilayani hapa.
“Hapa mnalalamika kuwa watumishi wanakimbia kazi mfano huko Kijiji cha Songambele, wakati mnajua hali iliyopo huko, ndugu zangu madiwani kaeni na ile jamii pale kuna vitisho vya ajabu mtu hawezi kuvumilia,” alisema.
Kwa upande wake Mbunge wa Kiteto, Emmanuel Papian (CCM), alisema Kata ya Songambele imekuwa na changamoto za muda mrefu kwa wa- tumishi kutishiwa maisha hali inayofanya kukimbia maeneo ya kazi na wengine kuomba uhamisho na wengine kutishia kuacha kazi.
“Kuna mtumishi mmoja alishindwa kulala na kuondoka usiku kutokana na vitendo hivyo nimezungumza na Jeshi la Polisi kuwakamata watu wanaotishia watumishi hao kwa imani za kishirikin,” alisema.
Diwani wa Kata ya Songambele, Abdallah Bundallah (CCM) alisema vitisho hivyo vimesababisha watumishi wa idara mbalimbali za kama elimu na afya kukimbia makazi yao kutokana na imani hiyo.
Aliiomba Serikali kuharakisha mazungumzo na wananchi hao kuacha vitisho hivyo kwani waathirika wakubwa ni wanafunzi na wagonjwa.