27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

Watumishi Kiteto wapata hofu ya ushirikina

72b0285101fd47ee71f8cb4814d811c1

Na MOHAMED HAMAD, KITETO

SERIKALI wilayani  Kiteto, mkoani Manyara, imewataka wananchi kuacha kuwatishia watumishi wa Serikali kwa imani  za kishirikina,  hali inayowafanya waogope na  kukimbia makazi yao.

Akizungumza katika ya Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya  ya Kiteto hivi  karibuni,  Ofisa  Utumishi wa  Wilaya  ya Kiteto,  Raphael Makoninda,  alisema  japo Serikali haiamini uchawi lakini imekuwa tishio  kwa baadhi  ya watumishi wilayani hapa.

“Hapa mnalalamika kuwa watumishi wanakimbia kazi mfano huko Kijiji cha Songambele, wakati mnajua hali iliyopo huko, ndugu zangu madiwani   kaeni  na  ile  jamii  pale kuna vitisho vya ajabu mtu hawezi  kuvumilia,” alisema.

Kwa upande wake Mbunge wa  Kiteto,  Emmanuel Papian (CCM),  alisema  Kata  ya Songambele  imekuwa na  changamoto  za muda  mrefu  kwa wa- tumishi  kutishiwa maisha  hali inayofanya  kukimbia   maeneo ya kazi na wengine kuomba uhamisho na wengine kutishia kuacha kazi.

“Kuna mtumishi mmoja alishindwa kulala  na  kuondoka usiku  kutokana na  vitendo hivyo  nimezungumza na Jeshi la Polisi kuwakamata watu  wanaotishia watumishi hao  kwa imani za kishirikin,” alisema.

Diwani wa Kata ya Songambele, Abdallah Bundallah (CCM) alisema vitisho hivyo vimesababisha watumishi wa  idara  mbalimbali za  kama elimu na afya kukimbia makazi yao kutokana na imani hiyo.

Aliiomba Serikali kuharakisha mazungumzo na wananchi  hao  kuacha  vitisho hivyo kwani waathirika wakubwa ni wanafunzi na wagonjwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles