24.8 C
Dar es Salaam
Saturday, May 28, 2022

Zungu amwomba radhi Mbowe

MWENYEKITI wa Bunge, Mussa Zungu.
MWENYEKITI wa Bunge, Mussa Zungu.

Na Maregesi Paul, Dodoma

MWENYEKITI wa Bunge, Mussa Zungu, amemwomba radhi Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, baada ya kutomtaja

alipokuwa akiwashukuru viongozi walioshiriki kuwapa pole waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Septemba 10 mwaka huu mkoani Kagera.

    Zungu alimuomba radhi Mbowe jana baada ya wabunge wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mwita Waitara wa Ukonga na Paschal Haonga wa Mbozi, kusimama na kuomba mwongozo kwa nyakati tofauti.

    Aliyeanzakumlalamikia Zungu ni Waitara ambaye katika maelezo yake, alisema anashangazwa na utaratibu uliotumiwa na mwenyekiti huyo wa Bunge kwa kushindwa kutambua mchango uliotolewa na Mbowe baada ya kutokea tetemeko hilo.

    “Mheshimiwa mwenyekiti, hivi punde umewataja na kuwashukuru viongozi mbalimbali wa Serikali walioshiriki kwa karibu kuwapa pole wananchi waliopatwa na matatizo kule Kagera kutokana na tetemeko la ardhi.

    “Umewataja waziri mkuu na mawaziri wengine walioshiriki tukio hilo, lakini hukumtaja kabisa kiongozi wa upinzani bungeni wakati naye alikwenda Bukoba kutoa pole.

    “Hata sisi wabunge wa Chadema kabla ya Bunge kukubali kukatwa posho ya siku moja ili kuwachangia waathirika, tulikuwa tumekwisha kuchangishana fedha na kumkabidhi mwenyekiti wetu azipeleke, lakini hukututaja.

    “Kwa hiyo, mheshimiwa mwenyekiti, naomba mwongozo wako juu ya tukio hili kwa vile imekuwa ni kawaida kwa viongozi wa Serikali kutowatambua viongozi wa upinzani katika matukio mbalimbali,” alisema Waitara.

   Hoja hiyo ya Waitara, iliungwa mkono na Haonga ambaye naye alionyesha kumshangaa Zungu kwa kutomtaja Mbowe.

    “Mheshimiwa mwenyekiti, mwongozo wangu hautofautiani na mwongozo wa Mheshimiwa Waitara kwa sababu umewataja viongozi wengine na kushindwa kumtaja Mbowe wakati ni kiongozi mkubwa hapa bungeni.

    “Kwa hiyo na mimi naomba mwongozo wako katika jambo hilo,” alisema Haonga baada ya kutumia kanuni ya 68 (7).

    Akijibu miongozo hiyo, Zungu alikiri kosa kwa kutomtaja Mbowe kwa kuwa naye alishiriki kwa karibu kuwapa pole waathirika wa tetemeko hilo.

    “Ni kweli sikumtaja Mbowe, namuomba radhi kwa kosa hilo. Hili suala lisitugawe, tuwe wamoja tuweze kuwasaidia ndugu zetu waliopata matatizo,” alisema Zungu.

    Awali, mwenyekiti huyo wa Bunge aliishukuru Serikali kwa jinsi ilivyoshiriki kwa karibu kukabiliana na madhara ya tukio hilo na kuitaka iendelee

na utaratibu huo kila majanga yanapotokea.

    Septemba 10 mwaka huu, tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 5.7 katika vipimo vya richter lilitokea mkoani Kagera na kusababisha vifo vya watu 17 na kujeruhi wengine zaidi ya 200.

    Pia, tetemeko hilo lilisababisha majengo na nyumba kadhaa kuharibiwa zikiwamo taasisi za umma na za binafsi.

    Wakati huo huo serikali imewasilisha miswada miwili bungeni kwa ajili ya kuimarisha shughuli za uvuvi na kilimo nchini.

    Miswada hiyo ya Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania ya Mwaka 2016 na Muswada wa Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania

wa Mwaka 2016, iliwasilishwa jana na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk. Charles Tizeba.

    Akiwasilisha Muswada wa Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania ya Mwaka 2016, Dk. Tizeba alisema sheria inayopendekezwa inakusudia kuweka mfumo wa utafiti unaolenga kuimarisha shughuli za utafiti wa kilimo kulingana na mahitaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,577FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles