25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Abiria watozwa viingilio feki Kituo cha Ubungo

img-20140423-wa0033

GRACE SHITUNDU Na ESTHER MNYIKA, DAR ES SALAAM

ABIRIA wa mabasi  ya kwenda mikoani na nchi jirani katika Kituo cha Ubungo  (UBT), wa- natozwa viingilio batili kiny- ume cha utaratibu.

Utaratibu unaojulikana abiria anapokuwa na tiketi hairuhisiwi kumtoza fedha  za kiingilio   ambayo   ni  Sh  300. Hata    hivyo,   hali   ni   tofauti kwani  watu  wote  wamekuwa wakitozwa fedha za viingilio. Wakizungumza na MTANZANIA kwa  nyakati  tofauti, abiria   hao   walisema  wameshangazwa  na  utaratibu huo,kwani  siku  zote  wanaposafiri huingia katika kituo hicho kwa kutumia  tiketi  za  mabasi  wanayosafiria.

Mmoja  wa  abiria  hao  Angela Yoredi  aliyekuwa  akisafiri kuelekea   Dodoma   na  basi  la ABC  alisema   ilimpasa   kulipia kiingilio cha Sh 200, licha kuonesha  tiketi   yake   mlangoni.

“Nashangaa imebidi nilipie Sh 200 wakati siku zote nikiwa na  tiketi  ya basi  ninapita bila kulipia, waliniambia huo ni utaratibu mpya unaotumika kwa sasa,” alisema Angela.

Naye  Mohamedi Issa  ambaye  alikuwa  anasafiri  na basi la   Hood   kwenda    Morogoro alisema    kwa   sasa   utaratibu wa   kuingia   katika   kituo   hicho  haueleweki,  kwani  awali watu   waliokuwa  wanalipa   ni wale waliokuwa wakiingia  kituoni  kwa  ajili ya  kupokea  au kusindikiza  abiria.

“Utaratibu wa humu sasa haueleweki  pale  mlangoni kuna abiria wanalipa  Sh 200 lakini mimi nililipa Sh 300 in- gawa  nilikuwa  tayari  na tiketi yangu ya basi,” alisema.

Akitoa ufafanuzi wa suala hilo, Ofisa  Uzalishaji,  Uratibu na Ushuru kituoni hapo, Novat Francis, alisema kitendo  hicho ni kinyume  cha sheria  na uta- ratibu  ambao  umepangwa katika kituo hicho.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles