27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Watumishi Housing yatakiwa kutumia force account katika miradi ya ujenzi

Na Mwandishi Weu, Dar es Salaam

Kamopuni ya Nyumba ya Watumishi Housing Company(WHC) imetakiwa kuacha kuendelea kutumia Wakandarasi katika miradi mbalimbali ya ujenzi wa nyumba za kuwauzia na kuwapangisha Watumishi wa Umma na badala yake watumie ‘force account’ ili kuokoa gharama na kujenga nyumba ambazo watumishi wataweza kupanga na kuzinunua.

Maelekezo hayo yametolewa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kufahamiana na watumishi wa Watumishi Housing Company ikiwa ni pamoja na kukagua miradi inayotekelezwa na taasisi zilizo chini ya ofisi yake.

Ndejembi amesema madhumuni ya kuanzishwa kwa Watumishi Housing Company ni kujenga nyumba za gharama nafuu zinazoweza kununuliwa na Watumishi wa kada zote, hivyo hakuna sababu ya kutumia wakandarasi ambao gharama zao za ujenzi ni kubwa na kusababisha gharama kubwa za upangishaji na uuzaji wa nyumba hizo.

“Watumishi wa Umma wanajitoa sana katika kulitumikia taifa hili, sasa ni wakati wa Serikali kutambua mchango wao kwa kuwawezesha ikiwa ni pamoja na kuwapatia nyumba za gharama nafuu,” Ndejembi amesisitiza.

Ndejembi ameongeza kuwa, kuna majengo mbalimbali ya Serikali yaliyojengwa kwa ubora kwa kutumia ‘force account’ na kutolea mfano wa baadhi ya majengo hayo ambayo yako katika Mji wa Serikali-Mtumba kuwa ni TARURA na TAMISEMI.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa WHC, Dk. Fredy Msemwa amesema wamepokea maelekezo ya Naibu Waziri ya kutumia ‘force account’ na wameshajiandaa kwa ajili ya hilo.

Ameongeza kuwa, walishaanzisha Kampuni ndani ya Watumishi Housing ambayo imetumika kujenga nyumba 61 na nyingine wanatarajia kuzijenga jijini Dodoma na Mwanza na maeneo mengine nchini.

Ujenzi wa miradi ya nyumba za Watumishi Housing kwa kutumia force account itahusisha njia ya ununuzi wa kazi ya ujenzi kwa kutumia taasisi ya umma au watumishi wake na vifaa au wafanyakazi wa kukodi, njia ambayo itawezesha Watumishi wa Umma kupanga au kununua nyumba kwa gharama nafuu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles