24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, April 14, 2024

Contact us: [email protected]

Watumishi Bukoba wamshukuru Rais Samia kwa kuwapandisha madaraja

Na Renatha Kipaka, Bukoba

Watumishi wa Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera wamemshukuru Rais Samia Sulu8hu Hassan kwa kuwaongezea mshara na kuwapandisha madaraja.

Kauli hiyo imetolewa juzi na Afisa Kilimo wa Kata ya Kitendaguro, Severine Leonard wakati akizungumza na Mtanzania Digital ambapo amesema kuwa Rais Samia ameondoa utofauti mkubwa uliokuwepo miongoni mwa watumishi nchini wale wa kima cha juu na cha chini.

Afisa Kilimo wa Kata ya Kitendaguro, Severine Leonard.

“Nitumie fursa hii kumpongeza Rais Samia Suluhu kwa kuwaona watumishi nchuni kwani kiwango hiki alichotuongezea kitatusaidia kupunguza ugumu wa maisha,” amesema Leonard.

Kwa upande wake, Afisa Uvuvi Manispaa ya Bukoba, Bhoke Thomas amesema kuwa anamshukuru Rais Samia kwa kuwakumbuka kwani nizaidi ya miaka mitano walikuwa hawajaongezwa mshahara wala kupandishwa vyeo.

Afisa Uvuvi Manispaa ya Bukoba, Bhoke Thomas.

“Hii ilikuwa inatupa wakati mugumu sana katika kuteketeza majukumu yetu kutokana na gharama za maisha kupanda ilihali kipato kikiwa pale pale, hivyo alichokifanya mheshikiwa Rais Samia kiukweli kimeturudidhaia matumaini na kutupa ari ya kufanya kazi kwa bidii,” amesema Thomas.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles