30.3 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Watumishi 1150 waliokosa sifa kulipwa stahiki zao

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Mohammed Mchengerwa amesema watumishi 1150 walioondolewa kwa kukosa sifa ambao hawajiendeleza watalipwa stahiki zao zote kutokana na maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Pia amewaagiza Wakurugenzi  wa Halmashauri  wawapokee taarifa za watumishi ambao baada ya kuondolewa kazini walienda kujiendeleza.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Novemba 2,2021, Jijini Dodoma kuhusu maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Mchengwerwa amesema wizara yake inatambua mchango wa kila mtumishi katika eneo lake hivyo iliamua kuwawajibisha ambao hawakuwa na sifa.

“Tunatambua mchango wa kila mtumishi katika eneo lake lakini ikumbukwe wizara hii inasimamia utawala bora kikubwa ni kusimamia sheria na taratibu msingi wa watumishi kuondolewa ni kutokana na kughushi baadhi ya vyeti.

“Lakini Rais wa awamu ya sita alisisitiza wapo watumishi ambao waliajiriwa kwa vigezo ambavyo awali havikuwa vimeongezwa vya elimu zao na wakaondolewa kazini zaidi ya watumishi 4185.

“Lakini kwa huruma ya Rais wetu wa awamu ya sita akatuagiza tupitie ili tuweze kujiridhisha ni watumishi wangapi ambao waliweza kujiendeleza, walipewa muda na kufikia mwaka 2020 wawe wamekidhi vigezo

“Nitoe taarifa kwamba kati ya watumishi ambao waliajiriwa na hawakuwa na elimu ya kidato cha nne na wengi wao ambao waliondolewa kazini kwa kigezo hicho, wale walioweza kujiendeleza zaidi ya watumishi 4100 tayari tumewarejesha kazini na pengine wapo ambao hawakuwahi kusikia agizo la serikali

“Nitumie jukwaa hili kuwaagiza wakurugenzi katika halmashauri waweze kupokea taarifa za watumishi ambao wanakidhi vigezo,”amesema.

 “Kwa hiyo watumishi zaidi ya 1495 wanapaswa kurejea kazini lakini katika idadi hiyo wapo watumishi takribani 1150 ambao wao hawakufanikiwa kujiendeleza maana yake hawana sifa za kutosha kuendelea kutumikia ndani ya Serikali japokuwa walikuwa ni watendaji wazuri.

Aidha Mchengerwa ameyataja mafanikio  yaliyopatikana katika miaka 60 ya  uhuru ni pamoja na kuongezeka kwa ajira katika utumishi wa umma kutoka watumishi 17,565 mwaka 1961 hadi 528,290 Oktoba 2021.

Amesema kati ya hao watumishi wa sekta ya afya wamefikia 72,961 sawa na asilimia 13.8 na walimu wamefikia 281,729 sawa na asilimia 53.3.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles