25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

Duka la TEHAMA lazinduliwa Dodoma

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

KAMPUNI ya Mhawa Net ICT imezindua duka la Teknolojia na Mawasiliano (TEHAMA) jijini Dodoma na kuishauri Serikali kuangalia upya bei za vifurushi vya ‘internet’ kwani gharama zimekuwa kubwa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka hilo katika eneo la Uhindini jijini Dodoma Mkurugenzi wa Mhawa Net ICT, Saimon Chagula amesema huu ni wakati muafaka kwa wakazi wa Dodoma kupata huduma zenye ubora.

“Nishauri Serikali kwenye suala la internet sasa hivi kuna changamoto kubwa ya gharama za bando ni kubwa kwa hiyo  waangalie kupunguza  ili kuwawezesha kila mmoja aweze kuperuzi mtandao.

“Lakini kuna changamoto ya anuani za makazi naomba mamlaka husika na mgawanyo wa anuani za makazi waweze kuifanyia kazi kwa haraka tuweze kurahisisha biashara ya mtandao.Kama unavyojua biashara ya mtandao huwezi kuwa na mtandao peke yake ‘address’ ndio muhimu

Chagula amesema  duka hilo litarahisisha  upatikanaji wa  huduma za mitandao huku ikiahidi kuongeza chachu ya  ufanisi katika ubunifu wa utoaji wa huduma kwa jamii na kufikia malengo ya  uchumi wa pamoja.

“Mbali na huduma nyingi tunazotoa,kampuni yetu itakuwa ikitoa ushauri wa matumizi bora na salama ya vifaa na mifumo ya TEHAMA,lakini pia tutatoa fursa ya ajira kwa vijana,”amesema.

Ameeleza kuwa ikiwa watanzania wengi watachochea maendeleo ya TEHAMA nchini,  uchumi wa kijiditali utakua kwa kasi na kurahisisha huduma za mitandao ambapo hivi sasa vitu vingi na malipo ya bili yanafanyika kwa njia ya mtandao.

Kwa upande wake mtaalam wa TEHAMA,Daniel  Natai, amepongeza ujio wa  kampuni  hiyo na kusema  ni fursa kwa wakazi wa Dodoma kwani itawapunguzia gharama za kusafiri hadi Dar es Salaam kufuta huduma hizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles