29.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Watuhumiwa ujambazi watano wauawa

WLEONARD MANG’OHA

-DAR ES SALAAM

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limewaua watu watano wakituhumiwa kujihusisha na ujambazi na kuwakamata wengine wanne akiwamo askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), Friday Kumingi (29), baada ya kukutwa na silaha kinyume cha sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, alisema katika tukio la kwanza Machi 3 mwaka huu saa 12:30 jioni huko maeneo ya Maili Moja, Kibaha mkoani Pwani polisi walimkamata askari huyo wa kikosi cha 36KJ Kibaha Msangani na katika mahojiano mtuhumiwa huyo alikiri kumiliki silaha mbili kinyume cha sheria.

Mambosasa alisema mtuhumiwa huyo alidai kuwa silaha hizo alikuwa anazihifadhi  nyumbani kwa mke wake mdogo Mtaa wa Muheza Kibaha na kwamba huzitumia katika matukio ya uhalifu katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam na Pwani.

“Baada ya mahojiano polisi na mtuhumiwa huyo walifika kwenye nyumba hiyo na kukamata silaha ya AK47 yenye namba NM174844 ikiwa na risasi 20 ndani ya magazini, boksi moja likiwa na risasi 27, bastola moja yenye namba 3249 ikiwa na risasi saba ndani ya magazini na risasi tatu za silaha ya kivita ya G3.

“Mtuhumiwa alikubali kuwaonyesha wenzake watatu anaoshirikiana nao katika matukio hayo na askari walipofika kwenye nyumba wanayoishi watuhumiwa hao walianza kukimbia kupitia mlango wa nyuma na hatimaye askari walirusha risasi hewani kuwaamuru wasimame lakini walikaidi na ndipo walipowafyatulia risasi za miguu ambazo ziliwajeruhi na walifariki dunia wakiwa njiani kupelekwa  hospitali” alisema Kamanda  Mambosasa.

Katika tukio jingine, Jeshi la Polisi limekamata silaha moja ya Shortgun iliyokatwa kitako na mtutu maeneo ya Mbondole Kata ya Kivule katika nyumba ya dereva wa  gari la Serikali lenye namba STL 301 mali ya Wakala wa Vipimo, Wilaya ya Kinondoni Christian Haule (39).

Mambosasa alisema Februari 06 mwaka huu saa 2:35 usiku Mtaa wa Narung’ombe na Likoma Kariakoo  mlinzi wa Kampuni ya Chim Risk Management,  Christian Mchagwa kwa kushirikiana na wezi walivunja stoo  na kuiba kisha kutoweka na silaha ya kampuni.

Katika tukio la tatu polisi jijini humo walikamata  bastola moja ya Chinese iliyofutwa namba na risasi mbili za silaha hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles