26.7 C
Dar es Salaam
Saturday, February 24, 2024

Contact us: [email protected]

Watu watano wafa ajali ya basi Mwanza

Ahmed Msangi
Ahmed Msangi

Na Judith Nyange, Mwanza

WATU watano wamefariki dunia na wengine 13 kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka   Dar es salaam kuja Mwanza,   mali ya Kampuni ya Super Sami kugonga mawe makubwa matatu yaliyokuwa yametegwa barabarani na watekaji.

Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana saa 7 usiku katika barabara ya Mwanza – Shinyanga eneo la Bushini Kata ya Mabuki wilayani Misungwi mkoani Mwanza.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi, alisema basi hilo lilipunduka baada ya kugonga jiwe kutokana  ni mwendo kasi.

Taarifa hiyo hiyo ilisema  baada ya dereva wa basi hilo aliyetajwa kwa jina la William Elias (45) mkazi wa Mabibo Dar es Salaam kugonga jiwe alishindwa kulimudu gari hilo ambalo lilipinduka  na kusababisha vifo vya watu watano akiwemo yeye mwenyewe pamoja na dereva wake msaidizi na kujeruhi abiria wengine 13.

“Waliofariki dunia katika ajali hiyo pamoja na dereva   Elias ni  Violeth Odede (21) mkazi wa Mwanza, mwanaume mmoja na wanawake wawili wenye umri wa miaka 25-30 ambao majina yao yalikuwa hayajatambuliwa.

“Majeruhi katika ajali hiyo ni Sophia Miraji anayekadiriwa kuwa na miaka 20-25, Kibilo Mwacha anayekadiriwa kuwa na miaka kati  ya 35-40, Boniphace Charles anayekadiriwa kuwa na miaka 38-40,  Frank Munyumi anayekadiriwa kuwa na miaka kati ya 25-30,

“Wengine ni Stanley Zacharia anayekadiriwa kuwa na umri kati ya 25- 30, Sia Dawson (28), Hellen Leheke anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 30- 35, Michael Leonard miaka kati ya 30- 35, Kudra Ibrahim mtoto wa miaka miwili na miezi sita, Zamda Issa (24), Marietha Christopher(26), Elizaberth Simon(40) na Dickson Msamba (22).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles