25.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

Watoto zaidi ya 700,000 kupewa chanjo ya surua-rubela, polio Tabora

ALLAN VICENT

Wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri nane za Mkoa wa Tabora wameagizwa kusimamia ipasavyo kampeni ya chanjo ya Surua-Rubella na Polio kwa watoto wenye umri wa kuanzia miezi tisa hadi miaka minne na miezi 11 na kuhakikisha wanafanikisha zoezi hilo kwa asilimia 100.

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa huo, Aggrey Mwanri katika uzinduzi wa kampeni ya siku tano ya chanjo hiyo inayotarajia kutolewa kwa watoto 489,193 kwa chanjo ya surua-rubella na watoto 213,148 wa chanjo ya polio.

Mwanri amewataka kusimamia ipasavyo fedha zilizotolewa na serikali  kiasi cha Sh milioni 497 kwa ajili ajili ya utekelezaji wa kampeni hiyo katika halmashauri zao na kusisitiza kuwa watumishi wa afya pamoja na waratibu watakaobainika kuwatoza fedha wananchi ili watoto wao wapatiwe chanjo hizo watachukuliwa hatua za kisheria.

Amesema serikali imekusudia kutoa chanjo hiyo bure pasipo malipo yoyote ili kukinga watoto hao na magonjwa mbalimbali, hivyo ni marufuku kwa watumishi kuomba fedha kwa wananchi.

Awali Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dk. Honoratha Rutatinisibwa amesema chanjo hiyo itatolewa kwenye vituo vya afya 466 vya serikali, watu binafsi na vituo vya muda vilivyoandaliwa na halmashauri husika.

 Amesema chanjo ya Surua-Rubella itawahusu watoto wenye umri wa miezi tisa hadi miaka minne na miezi 11 ambapo chanjo ya Polio ya sindano itawahusu watoto wote wenye umri wa mwaka mmoja na nusu hadi miaka mitatu na nusu.

Dk. Rutatinisibwa amesema chanjo hiyo imelenga kuwakinga watoto hao dhidi ya magonjwa ya mtoto wa jicho, matatizo ya moyo, kutokusikia vizuri, mtindio wa ubongo, matatizo ya ukuaji na kupooza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles