WATATU KIZIMBANI KWA UNYANG’ANYI WA SILAHA

0
626

ERICK MUGISHA na PATRICIA KOMBA (SAUT) – DAR ES SALAAM

WATU watatu wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kwa kosa la Unyang’anyi wa kutumia silaha.

Mwendesha Mashtaka wa Jamuhuri Ellen Masulali alidai mshtakiwa wa kwanza na wa pili hawakufika mahakamani na kuomba kusomewa mshtakiwa wa tatu mashtaka na kutajwa tarehe nyingine kwa washtakiwa ambao hawakufika mahakamani, Aliyefika Mahakamani ni Mkazi wa Tegeta kilimahewa, Kharidi Mafutaa (26).

Mwendesha Mashtaka wa Jamuhuri Masulali alimsomea hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Happiness Kikoga, alidai Julai 12 mwaka huu eneo la Bunju Wilayani Kinondoni, Dar es salaam waliiba simu mbili aina Samsung j7 pro yenye thamani ya sh 750,000 na Samsung A50 yenye thamani ya sh 950,000.

Cheni ya dhahabu yenye thamani ya sh 350,000 na fedha taslimu sh 1,000,000. Mali ya Jesca Nasari, kabla na baada walimtishia kwa panga Jesca Nasari ilikujipatia mali hizo.

Mshtakiwa alikana kutenda shtaka na Mwendesha Mashtaka wa Jamuhuri alidai Upelelezi hauja kamilika na kuomba mahakama tarehe nyingine kwa kutajwa.

Hakimu kikoga alisema kwa muujibu wa sheria na kanuni la kosa hilo mshtakiwa hatakuwa anatokea rumande hadi mwisho wa kesi kwa kutokuwa na dhamana na kesi itatajwa tena Octoba 29.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here