Bajaji ya abiria sita yazinduliwa

0
1008

MWANDISHI WETUDAR ES SALAAM

Bajaji internation kupitia kwa wasambazaji wake nchini Tanzania, Sunbeam Auto ltd imezindua usafiri wa miguu mitatu ‘Bajaji’ aina ya Maxima Z Hyyat Regency jijini Dar es salaam, yenye uwezo wa kubeba abiria sita na dereva.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa mauzo Bajaji Tanzania, Jestas Kyolike amesema uzinduzi huu wa bajaji mpya umekuja kuondoa shida ya usafiri kwa abiria wengi hapa nchini kwani bajaji hizo zina uwezo wa kubeba abiria zaidi ya wanne na mizigo mikubwa.

“Bajaji hizi ni imara na husaidia kwenye kipindi cha mvua maana imezibwa juu  pia ni bajaji ambayo ina umbo dogo lakini inauwezo wa kubeba abira, mizigo na inapita aina yoyote ya barabara nzuri au mbaya kutokana na kuwa na vifaa imara,”.

“Wito wangu kwa watu ambao hawana ajira wanatakiwa wafike kwenye ofisi zetu na kuwapa maelekezo ya kuweza kupata mkopo wa chombo kupitia benki zetu za hapa nchini kwa kulipa kidogo kidogo hadi mwisho wa mkopo wako kwa kufuata vigezo na masharti,” amesema Kyolike.

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Bajaji, Dinesh Kulyarni amesema wameamua kuleta bidhaa hiyo nchini wakiamini kuwa itawafaa wateja wao kwakuwa inatumia mafuta kidogo.

“Tumeona tulete usafiri huu Tanzania kwasababu tunaamini itawafaa sana wateja wa hapa na ina uwezo wa kukunja viti vya abiria na ukaweka mizigo mingi kwa kuwa ina nafasi kubwa”, amesema Kulyarni.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here