25.5 C
Dar es Salaam
Thursday, December 12, 2024

Contact us: [email protected]

Watoroshaji wa mifugo nje ya nchi watangaziwa kiama

Na Abel Paul wa Jeshi la Polisi Arusha

Kamanda wa Kikosi cha kuzuia wizi wa Mifugo Tanzania Kamishina Msaidizi wa Polisi ACP Simon Pasua ametangaza kiama kwa watu wanaotorosha mifugo kwenda nje ya nchi nakwamba hata muonea muhali atakayebainika kufanya hivyo.

ACP Pasua ametoa onyo hilo leo Jumatatu Juni 6, 2022 wakati akizungumza na Askari wa kikosi hicho Makao Makuu ya kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo (STPU) jijini Arusha.

Amesema zipo taarifa za watu wachache wanaojihusisha na utoroshaji wa mifugo nje ya nchi, ambapo amesema kikosi hakitomuonea muhali mtu yeyote anayetorosha mifugo kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Mkuu huyo wa kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo Tanzania amewataka watendaji wa kikosi hicho kutojihusisha kwa namna yoyote na watuhumiwa wenye lengo la kutorosha mifugo.

Kamanda wa Kikosi cha kuzuia wizi wa Mifugo Tanzania, Kamishina Msaidizi wa Polisi ACP Simon Pasua.

“Nitoe onyo kwa wale wote ambao wanajihusisha na kutorosha mifugo nje ya nchi kinyume na utaratibu kwamba iwapo watabainika hatutasita kuwachukulia hatua kali za kisheria.

“Lazima watu watambue kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria lakini pia kama haitoshi inapunguza pato la taifa,” amesema ACP Pasua.

Aidha, katika hatua nyingine ACP Pasua amewasihi wafugaji kote nchini kufuata taratibu ya uuzaji wa mifugo yao ili kuongeza pato lao na taifa kwa ujumla.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles