29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

WATATU AZAM KUIKOSA NJOMBE MJI

Na ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM

AZAM FC inatarajia kuwakosa wachezaji wake watatu, Himid Mao, Daniel Amoah na Yakubu Mohamed, itakapoumana na Njombe Mji katika mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Sabasaba, Njombe.

Wachezaji hao wataukosa mchezo huo kutokana na kuwa na kadi tatu za njano walizozipata kwenye michezo ya timu hiyo iliyopita.

Akizungumzia mchezo huo, Kocha Mkuu wa Azam FC, Aristica Cioaba, alisema anaamini kikosi chake kitapata ushindi na kujiweka katika mazingira mazuri zaidi ya kufikia matarajio yao ambayo ni kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

“Kila mechi ni tofauti, kimsingi tunakwenda kupambana ili malengo yetu yatimie, ingawa lazima tukiri kwamba haitakuwa rahisi kwa kuzingatia kila mmoja anataka kushinda nyumbani,” alisema Cioaba.

Akizungumzia hatua ya kuwakosa wachezaji hao muhimu, alisema ana kikosi kipana ambacho kina uwezo wa kupambana na kupata matokeo mazuri.

Azam ipo nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ikiwa imejikusanyia pointi 19, sawa na vinara Simba, walioko kileleni kutokana na kigezo cha wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles