24.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

LUKAKU AWEKA HISTORIA YA UFUNGAJI UBELGIJI

BRUGES, UBELGIJI

MSHAMBULIAJI wa timu ya Taifa ya Ubelgiji, Romelu Lukaku, ameweka historia mpya ya kuwa mchezaji namba moja anayeongoza kwa mabao katika Taifa hilo baada ya juzi kupachika bao kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Japan.

Katika mchezo huo ambao ulipigwa kwenye uwanja wa Jan Breydel, mjini Bruges, wenyeji Ubelgiji walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0, lililofungwa na mshambuliaji huyo katika dakika ya 72.

Bao hilo limemfanya Lukaku kuwa mchezaji wa kwanza kuwa na mabao mengi katika timu hiyo ya Taifa kwa kipindi chote, akiwa na jumla ya mabao 31 tangu aanze kuitumikia timu huyo mwaka 2010 akiwa amecheza jumla ya michezo 65.

Lukaku alifanikiwa kufunga bao hilo baada ya kazi safi iliyofanywa na mchezaji mwenzake, Nacer Chadli, kwa kupiga pasi ya juu ambayo ilimaliziwa kwa umakini wa hali ya juu na Lukaku ambaye anakipiga katika klabu ya Man United.

Kabla ya bao la Lukaku katika mchezo wa juzi, alikuwa sawa na mchezaji wa zamani wa timu hiyo, Bernard Voorhoof ambaye alikuwa na jumla ya mabao 30 baada ya kucheza soka tangu mwaka 1928 hadi 1940 alipotangaza kustaafu.

Wachezaji wengine ambao wameingia kwenye orodha ya wafungaji bora kwa kipindi chote ni pamoja na Paul Van Himst, aliyekuwa na jumla ya mabao 30 baada ya kucheza soka tangu mwaka 1960 hadi 1974, Joseph Mermans akifunga mabao 28 tangu mwaka 1945 hadi 1956, Marc Wilmots, akipachika mabao 28 tangu mwaka 1990 hadi 2002.

Wengine ni Robert De Veen, akifunga mabao 26 kuanzia mwaka 1906 hadi 1913, Wesley Sonck akifunga mabao 24 kuanzia 2001 hadi 2010, huku Ray Braine akifunga mabao 23 kuanzia mwaka 1925 hadi 1939 na Marc Degryse akifunga mabao 23 kuanzia mwaka 1984 hadi 1996.

Lukaku mbali na kuweka rekodi hiyo nchini Ubelgiji, lakini amekuwa na kipindi kigumu ndani ya klabu yake ya Man United kutokana na baadhi ya mashabiki wakidai mchezaji huyo amekuwa na uwezo mdogo katika safu yake ya ushambuliaji japokuwa anaongoza kwa kupachika mabao akiwa na jumla ya mabao saba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles