24.7 C
Dar es Salaam
Saturday, April 13, 2024

Contact us: [email protected]

AJIB AONJA HASIRA ZA LWANDAMINA

Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Ibrahim Ajib, jana alionja hasira za kocha wake, George Lwandamina, baada ya kupewa adhabu ya kupiga pushapu za kutosha.

Tukio hilo lilitokea wakati wa mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Tukio lenyewe lilikuwa hivi, Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina, aliwataka wachezaji wa timu hiyo  kukimbia, ikiwa ni utaratibu wake wa kawaida kabla ya kuhitimisha mazoezi.

Wachezaji wa timu hiyo walitii agizo la kocha wao kwa kuanza kukimbia, lakini Ajib hakufanya hivyo, badala yake alikuwa akitembea.

Hatua hiyo ilimkera Lwandamina, ambaye alimtaka Ajib apige pushapu, mshambuliaji huyo alitii kwa kupiga pushapu tano kisha kuinuka na kuanza kukimbia.

Hata hivyo, Lwandamina hakuridhika, hivyo akamtaka aendelee kupiga pushapu, ambapo mchezaji huyo aliongeza nyingine tano kisha akasimama na kuendelea na zoezi la kukimbia pamoja na wachezaji wenzake.

Ajib amekuwa mchezaji tegemeo katika kikosi cha Yanga tangu alipojiunga na timu hiyo wakati wa dirisha la usajili la msimu huu akitokea Simba.

Tayari fowadi huyo wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) ameifungia Yanga  mabao matano katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles