23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

BIRDMAN AMJIBU RICK ROSS

NEW YORK, MAREKANI

KIONGOZI wa kundi la Young Money Cash Money Records, Bryan Williams ‘Birdman’, amemjia juu rapa mwenzake Rick Ross baada ya msanii huyo kutumia ukurasa wake wa Instagram na kumwambia kiongozi huyo alipe deni lake kwa Lil Wayne.

Lil Wayne amekuwa na mgogoro mkubwa na kiongozi huyo kutokana na kudai kiasi cha fedha cha dola milioni 51 baada ya kufanya kazi pamoja kwenye lebo hiyo ya muziki, kutokana na hali hiyo Lil Wayne akaamua kujitoa kwenye kundi hilo na kutaka alipwe fedha zake.

Rick Ross ambaye amekuwa rafiki wa nyota hao wawili, sasa anaonekana kuegemea upande mmoja na kumtaka Birdman alipe deni kwa Lil Wayne.

Rick Ross aliandika kwenye ukurasa wa Instagram: “Lil Wayne anatakiwa kulipwa chake kutokana na kile alichokifanya ndani ya mkataba wake.” Kauli hiyo imemchukiza Birdman na kuamua kumjibu kwa kusema: “Fuata yako, kila mmoja na maisha yake hakuna haja ya kuingilia mambo usiyoyajua.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles