23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, May 18, 2024

Contact us: [email protected]

JORDIN SPARKS AFUNGA NDOA KIMYAKIMYA

NEW YORK, MAREKANI

NYOTA wa filamu na muziki nchini Marekani, Jordin Sparks, amewashangaza mashabiki wake kwa kufunga ndoa kimyakimya na kuzisambaza picha zake kwenye mitandao ya kijamii.

Staa huyo ambaye alitamba na wimbo wake wa ‘No Air’ aliyomshirikisha mkali wa RnB, Chris Brown, mbali na kufunga ndoa hiyo kimyakimya lakini pia amethibitisha kuwa na ujauzito.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, mrembo huyo ambaye alianzia muziki kwenye mashindano ya American Idol na kutwaa taji la mashindano hayo, ameiweka picha ya harusi akiwa na mpenzi wake Dana Isaiah.

Inadaiwa harusi hiyo ilifungwa mapema Julai mwaka huu, lakini waliamua kuifanya siri na sasa wameamua kuweka wazi na kudai wanatarajia mtoto wao wa kwanza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles