23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

DIAMOND, VANESSA KUTUMBUIZA TAMASHA LA ONE AFRICA MUSIC

NA CHRISTOPHER MSEKENA

WASANII wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, Vanessa Mdee na Dj D Ommy, leo wanatarajia kuungana na mastaa wengine wa Afrika kudondosha burudani ya nguvu katika tamasha la One Africa Music linalofanyika Falme za Kiarabu, Dubai.

Tamasha hilo lenye lengo la kuwakutanisha mashabiki wa muziki wa Afrika popote pale duniani, huwa linafanyika kila mwaka ambapo mwaka uliopita lilifanyika katika Uwanja wa Barclays Center, Brooklyn nchini Marekani na leo linafanyika kwenye Uwanja wa Madinat Arena, Dubai.

Mbali na Diamond Platnumz, Vanessa Mdee na Dj D Ommy, wasanii wengine watakaokonga nyoyo za mashabiki ni pamoja na Davido, Wizkid, Sarkodie, Betty G, Edel Ebrahim, Mr Flavour, Tiwa Savage, Victoria Kimani, Cassper Nyovest, 2 Face, Banky W na Sauti Soul.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles