27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Watanzania 25 wakamatwa nje kwa ‘unga’

Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Anthony Mavunde
Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Anthony Mavunde

Na GABRIEL MUSHI, DODOMA

WATANZANIA 25, wamekamatwa nje ya nchi kwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya mwaka 2015.
Kauli hiyo imetolewa jana mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Anthony Mavunde, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu taarifa ya hali ya dawa za kulevya kwa mwaka 2015.

Kwa mujibu wa Mavunde, Watanzania hao walikamatwa katika nchi za China (13), Brazil (9) na Zambia (3) ingawa hadi sasa hakuna aliyenyongwa kwa tuhuma hizo.

“Taarifa imebainisha kuwa mwaka 2015 biashara ya dawa za kulevya iliendelea kufanyika kwa kiwango kikubwa, huku nchi ikishuhudia kuibuka tena kwa biashara ya mandrax baada ya kukamatwa kwa kilo 5.1 za dawa hizo mkoani Dodoma na Ruvuma. Dawa za aina hiyo zilikamatwa kwa mara ya mwisho mwaka 2010.

“Wanaume wameendelea kuwa wahusika wakuu wa biashara hii, ingawa takwimu zinaonyesha pia wanawake nao wanajihusisha na biashara hiyo kwani kati ya watu 15,815 waliokamatwa nchini kwa tuhuma hizo, wanawake walikuwa 1,436.

“Idadi hii ni kubwa hasa ikizingatiwa wanawake kiutamaduni ni watu wanaoaminika kwa kutokuwa na kawaida ya kujihusisha na vitendo vya uhalifu,” alisema Mavunde.

Pamoja na hayo, alisema matumizi ya bangi nchini yameshuka ingawa biashara hiyo imeendelea kushika kasi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles