22.5 C
Dar es Salaam
Friday, June 21, 2024

Contact us: [email protected]

Auawa baada ya kuiba kondoo

522_4687

Na IBRAHIM YASSIN, SONGWE

JOSEPH Salanga (30), mkazi wa Kitongoji cha Mbugani, Kijiji cha Songambele, Kata ya Magamba wilayani Songwe, Mkoa wa Songwe, ameuawa na watu wasiofahamika kwa tuhuma za wizi wa kondoo ikiwa ni mali ya mkazi wa Songambele, aliyefahamika kwa jina moja la Songambele.

Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Songambele, Daniel Nzuri, alithibitisha kutokea kwa kifo hicho.

“Nilipokea taarifa kutoka kwa wananchi juzi, saa 12 alfajiri juu ya uwepo wa taarifa za kifo hicho.

“Nilichokifanya baada ya kupokea taarifa hizo, nilitoa taarifa katika Kituo cha Polisi Galula, ambapo askari polisi walifika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu na kuupeleka katika Kituo cha Afya Mbuyuni ambako ulifanyiwa uchunguzi.

Naye Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Songwe, Mathius Nyange, alikiri kupokea taarifa hizo.

“Tukio hilo lipo kwani baada ya kupata taarifa hizo, nilituma polisi ambao walikwenda eneo la tukio.

“Kwa sasa upelelezi unaendelea ili kuwabaini na hatimaye kuwakamata waliohusika katika mauaji hayo,” alisema Kamanda Nyange.

Pamoja na hayo, Kamanda Nyange alitoa wito kwa wananchi akiwataka watoe ushirikiano wa kuwakamata waliohusika katika tukio hilo.

Pia, aliwataka wananchi wasipende kujichukulia sheria mkononi kwa kuwa kufanya hivyo ni kosa kisheria na kwamba yeyote atayekamatwa baada ya kujichukulia sheria mkononi, atachukuliwa hatua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles