27.9 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Kiba kurudishiwa tuzo yake

Ali Kiba
Ali Kiba

Na BEATRICE KAIZA-DAR ES SALAAM  

MSANII nguli wa muziki wa kizazi kipya, Ali Kiba, anatarajia kurudishiwa tuzo ya msanii bora wa kiume ‘Best African Act’ iliyotolewa kimakosa kwa Wizkid wa Nigeria katika tuzo za MTV Europe Music Award 2016.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Meneja wa Kiba, Seven Moshi, alisema wamepokea taarifa kuhusu tuzo hiyo kutoka kwa MTV EMA.

 

“Taarifa za tuzo kukosewa ni kweli, Kiba alitakiwa kukabidhiwa yeye, lakini wasimamizi walijichanganya na kumpa Wizkid.

 

Moshi alisema tayari MTV EMA wamewasiliana na Wizkid  na amekubali kurudisha tuzo hiyo ili akabidhiwe Kiba.

 

“Tunasubiri tuzo irudishwe kwa MTV EMA ili sisi tukaichukue na kuileta nyumbani, jambo la kujivunia kuona msanii wetu ameshinda na tumekubali kuwa walifanya makosa,” alisema Moshi.

 

Moshi alieleza kuwa, tayari msanii Wizkid amefuta taarifa zote alizokuwa ametuma katika mitandao ya kijamii, zikionyesha kuwa yeye ndiye mshindi wa tuzo hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles