22.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Watakaorubuni watoto kufeli mitihani kukiona

Mwandishi wetu -Tandahimba

WAZAZI watakaowashawishi watoto wao wanaotarajia kufanya mitihani ya darasa la saba wiki ijayo kujaza majibu ya uongo ili wasifaulu kwa madai wana uwezo mdogo watachukuliwa hatua za kisheria.

Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake jana, Ofisa Elimu Msingi Wilaya ya Tandahimba, Hadija Mwinuka, alisema hatua za kisheria zitachukuliwa ili kukomesha tabia hiyo kwa wazazi.

“Tutawachukulia hatua wazazi watakaowashawishi watoto wao waandike majibu ya uongo, majibu yakitoka tutaangalia. Hii ni changamoto kwetu kwa kuwa wanawakatisha tamaa watoto na walimu ambao wanatamani wanafunzi wanaowafundisha wafaulu katika viwango vizuri,” alisema Mwinuka.

Alisema baadhi ya shule walimu wakuu wametoa taarifa ya kuwapo tabia hiyo, ambazo wanafikishiwa na wanafunzi wenyewe na hata mama wa watoto hao wakidai kina baba ndio hawataki watoto wafaulu.

“Sisi elimu wilaya tunapopata taarifa kama hizo kutoka kwa walimu wakuu, tunawaita wazazi wa sehemu husika na kuongea nao, endapo bado vitendo vitaendelea, hatuwezi kuwaacha, sheria itachukua mkondo wake,” alisema Mwinuka.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Ng’ongolo, Hawa Mzanda, alithibitisha kutokea tatizo hilo katika shule hiyo.

“Hii inakuwa ni changamoto hata kwa sisi walimu, maana tunapofundisha tunategemea wanafunzi wetu waelewe na wafaulu katika mitihani yao, linapokuja suala la wazazi kuwakatisha tamaa watoto na kuwaambia wajaze majibu ya uongo hata sisi walimu wanatuvunja moyo,” alisema mwalimu Mzanda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles