24.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 27, 2024

Contact us: [email protected]

Miradi ya Sh bil 26 Mbeya kutembelewa na Mwenge

Eliud Ngondo -Mbeya

MIRADI 59 yenye thamani ya Sh bilioni 26.3 itatembelewa wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru mkoani Mbeya.

Kati ya hiyo, 13 itazinduliwa na mingine kuwekewa jiwe la msingi na baadhi kukabidhiwa kwa walengwa.

Akizungumza jana wakati wa makabidhiano ya mbio hizo katika Kijiji cha Kambikatoto, Wilaya ya Chunya, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila alisema miradi hiyo yote, fedha za Serikali zilizotumika ni Sh bilioni 20.5, nguvu za wananchi Sh bilioni 2.1 Mfuko wa Jimbo Sh milioni 28.5 na fedha za wahisani Sh bilioni 2.3.

Katika mbio hizo ambazo ujumbe wa mwaka huu ni “maji ni haki ya kila mtu, tutunze vyanzo vyake na tukumbuke kushiriki Uchaguzi wa Serikali za mitaa”, baadhi ya miradi imewekewa jiwe la msingi na kuzinduliwa Wilaya ya Chunya.

Miradi hiyo ni pamoja na kufunguliwa katika Kijiji cha Lupa, kuweka jiwe la msingi Kijiji cha Ndalambo, nyumba ya walimu na shule ya sekondari Momba.

Mingine ni kuweka jiwe la msingi vyumba vya maabara Shule ya Sekondari ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kuzindua huduma ya umeme Kijiji cha Chipaka.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru, Mzee Ali Mkongea alisema Serikali imejitahidi kuwekeza katika miradi, hivyo wananchi wanatakiwa kuendelea kuitunza.

Mkongea alisema Serikali imeweza kutoa fedha katika ujenzi wa vituo vya afya na utoaji elimu bure ili kuweza kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora kwa lengo la kuijenga nchi.

Alisema wananchi wanatakiwa kujitokeza katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu ili kuwapata viongozi bora watakaosaidiana na Serikali kuleta maendeleo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles