Wastara: Hakuna kazi rahisi duniani

0
1330

WastaraNA SHARIFA MMASI, DAR ES SALAAM
MWIGIZAJI I wa filamu nchini, Wastara Juma, amesema wale wote wanaofikiri sanaa ya kuigiza ni kazi rahisi, wamekuwa wakijidanganya.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Wastara alisema katika dunia hakuna kazi nyepesi kwa sababu kila utakachokifanya kitahitaji matumizi ya akili na kufikiri.
“Kwa haraka haraka unaweza kusema kazi ya kuigiza ni nyepesi, lakini si kweli, lazima kila mmoja afahamu duniani kila kazi ina ugumu wake,” alisema Wastara.
Wastara alisema ugumu ambao wamekuwa wakikumbana nao waigizaji ni kucheza nafasi ambazo ni ngumu, tena kwa ubora zaidi wakati hawana ujuzi wala uzoefu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here