28.1 C
Dar es Salaam
Monday, November 29, 2021

Maandalizi Tamasha la Pasaka yamvutia Mfutakamba

Mfutakamba(2)(1)NA ELISHEBA NDIJENYEN, TUDARCO
MLEZI wa Tamasha la Pasaka, ambaye pia ni Mbunge wa Igalula kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Athumani Mfutakamba, amevutiwa na maandalizi mazuri ya tamasha la mwaka huu.
Waandaaji wa tamasha hilo, Kampuni ya Msama Promotion ya Dar es Salaam, wamepanga mwaka huu liwe tamasha la aina yake kwa ajili ya kusherehekea miaka 15 tangu lianzishwe.
Akizungumza Dar es Salaam juzi, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama, alisema Mfutakamba anaamini tamasha la mwaka huu litakuwa tofauti na yale yaliyopita nyuma.
“Yeye ni mlezi wa tamasha hili, ameona namna gani tunavyoshirikiana kusaidia jamii, tuna kila sababu ya kutembea kifua mbele,” alisema Msama.
Kwa mujibu wa Msama, wanataka tamasha la mwaka huu lionyeshe vitu vipya zaidi, ambavyo vitaacha historia tangu kuanzishwa kwake.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,324FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles