Dude kutoa elimu zaidi kwa wanafunzi

0
1438

dudeNA THERESIA GASPER, DAR ES SALAAM
MWIGIZAJI wa filamu za Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’, amesema yeye kama kioo cha jamii hana budi kutumia muda wake kuelimisha wanafunzi ili waweze kufanya vizuri katika masomo yao.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Dude alisema amekuwa akiwahamasisha wanafunzi, kupitia zawadi kama madaftari, vitabu, viatu hata sare za shule.
“Kama unavyojua mtoto unapompatia zawadi na kumuahidi mambo mazuri, lazima atajitahidi, nitaendelea kutembelea shule mbalimbali kuhamasisha masomo,” alisema Dude.
Dude alisema ana imani malengo aliyoweka yatawasaidia wanafunzi wengi ambao wamekuwa wagumu kupenda masomo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here