Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM
JINA la kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stephen Masato Wasira, bado linavuma ndani ya chama hicho, ambapo sasa limeibuka tena na kuonekana kuwa ni miongoni mwa wanaowania ujumbe wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC) kupitia kundi la kapu (Bara).
Wasira ambaye pia alikuwa ni mmoja wa mawaziri waliohudumu wizara mbalimbali katika Serikali ya Awamu ya Nne chini ya Rais Jakaya Kikwete, anatajwa kuwa ni mwanasiasa aliyedumu kwa muda mrefu tangu utawala wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.
Kwa mujibu wa orodha iliyotolewa juzi na Katibu wa NEC (Itikadi na Uenezi) wa CCM, Humphrey Polepole  jina la Wasira likiwa namba 23 katika orodha ya wajumbe wanaowania nafasi 15 za NEC katika kundi hilo.
Mbali na Wasira ambaye katika uchaguzi wa CCM mwaka 2012, alifanikiwa kushinda nafasi hiyo kwa kuwa wa kwanza nyuma ya January Makamba na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe.
Katika orodha hiyo ya nafasi 15 za kapu mbali na Wasira wengine wanaochuana kuwania ujumbe wa NEC kwa upande wa bara ni Rehema Peter Mroso, Anna Agatha Msuya, William Sarakikya, Angella Akilimali, Burton Kihoka Limuliko, Dk Ibrahim Msengi, Dk. Fenela Mukangara, Jerry Silaa.
Wengine ni Emmanuel Kamara, Neema Majule, Emanuel Shilole, Ashery Mndaula, Theresia Mtewele, Dk. Ladislaus Batinoluho, Hafsa Galitano, Charles Shenda, Shida Kanyengele, Rocky Mgeju, Nistas Mvungi, Shanel Ng’unda, Sofia Feruzi na Gaudence  Ngasa.
Orodha kamili ya walioteuliwa soma Ukurasa wa 8