24.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

WARIOBA: WANAMBEZA LAKINI AMETOA MCHANGO MKUBWA ZIMBABWE

AZIZA MASOUD Na AGATHA CHARLES – DAR ES SALAAM


WAZIRI Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba, amesema ingawa baadhi ya watu wanazungumza kwa kumbeza Rais Robert Mugabe baada ya kujiuzulu, mchango alioutoa kwa Zimbabwe ni mkubwa.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Jaji Warioba alisema  yaliyotokea Zimbabwe ni mabadiliko, lakini yamekuwa faraja kwakuwa yamefanyika kwa amani na kuiacha nchi ikiwa na utulivu.

“Hatua ya kujiuzulu kwa Mugabe imetokana na matatizo yaliyopo kwenye chama chake (ZANU-PF) kwa muda mrefu sasa, hata kabla ya Uhuru. Mara ya kwanza walikuwa na chama kimoja, lakini vurugu zilifanya wapate vyama viwili vya ZANU na ZAP, nadhani kwa sasa la muhimu ni nchi hiyo ipo salama,” alisema Jaji Warioba.

Aliongeza kuwa pamoja na kiongozi huyo kujiuzulu, mchango wake aliutoa kwa nchi hiyo ni mkubwa na hata kipindi alipokuwa akipigania uhuru aliwahi kukaa jela miaka 10.

“Amejiuzulu watu wanaongelea kwa hisia tofauti, lakini mimi naona mchango wake alioutoa kwa taifa la Zimbabwe ni mkubwa, kilichotokea kwake kinachangiwa na tatizo  la viongozi kukaa madarakani kwa muda mrefu, hatua aliyochukua ni nzuri kwakuwa katoka kistaraabu bila kupoteza utu wake,” alisema Jaji Warioba.

Alisema Mugabe na Mnangagwa walishiriki kikamilifu kutatua matatizo mbalimbali yaliyopo ndani ya nchi hiyo.

 

WASOMI NAO WASEMA YAO

Kwa upande wake, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Bashiru Ally, alisema anaamini Zimbabwe itaendelea na mapambano ya kiuchumi hata kama Mugabe hayupo madarakani.

“Kwa sasa Zimbabwe inatakiwa kuendelea kujipanga na mapambano dhidi ya uchumi, Mugabe yeye alifanya kazi ya kuikomboa nchi hiyo kisiasa, akafanya makosa katika nyanja za uchumi, basi watakaoiongoza kwa sasa ni jukumu lao kutekeleza suala hilo,” alisema.

Alisema uchumi wa nchi hiyo kwa sasa umeharibika kutokana na kuwapo kwa vikwazo vingi ambavyo viliwekwa na Mugabe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles