33.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

Wasifu wa Samia Suluhu Hassan : Rais wa kwanza Mwanamke Tanzania

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Samia Suluhu Hassan anakuwa Rais wa kwanza mwanamke nchini Tanzania. Samia anashika wadhifa huo baada ya kuhudumu kama Makamu Rais na kwa mujibu wa katiba, kufuatia kifo cha Rais Dk. John Pombe Magufuli ambapo anatakiwa kisheria kushika wadhifa wa urais.

Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akipigiwa mizinga 21 muda mcheche baada ya kuapishwa.

Samia Suluhu Mwanasiasa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) alizaliwa Zanzibar Januari 27, mwaka 1960.

Nyanja ya Siasa

Rais Samia aliianza safari yake ya kisiasa Mwaka 2000 alipochaguliwa katika Baraza la Wawakilishi la Zanzibar kama Mwakilishi wa kiti maalum na kuteuliwa na kushika wadhifa wa uwaziri na Rais wa Zanzibar wakati huo, Amani Karume, akiwa Mwanamke pekee katika nafasi ya juu ya uwaziri katika baraza hilo la mawaziri.

Mwaka 2010 Rais Samia akaona ni vyema kuwania ubunge katika bunge la Jamhuri ya Muungano ambapo alishinda kiti cha jimbo la Makunduchi kwa kupata takriban asilimia 80 ya kura.

Safari yake katika uongozi wa serikali ilianzia pale ambapo alichaguliwa na Rais Jakaya Kikwete mwaka 2014 kuwa Waziri wa nchi katika masuala ya muungano. Wakati Tanzania ilipokuwa katika mchakato wa kujadili katiba mpya ya nchi alichaguliwa kuwa makamu mwenyekiti wa bunge la katiba na kushiriki jukumu muhimu la kuandika rasimu ya katiba mpya.

Samia alisoma katika shule za Ng’ambo na Lumumba mjini Unguja, baadaye alijiunga na Taasisi ya Utawala wa Fedha ZIFA kwa masomo ya takwimu. Baada ya masomo hayo aliajiriwa katika wizara ya mipango na maendeleo na baadaye kujiunga na Chuo kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro. Alihudhuria pia masomo ya juu katika Chuo Kikuu cha Manchester huko London, Uingereza na kupata shahada ya uchumi na pia amesoma katika chuo kikuu cha New Hampshire, Marekani.

Hayati Dk. John Pombe Magufuli enzi za uhai wake.

Rais Samia aliteuliwa kushika wadhfa wa Makamu Rais wa 10 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye alishika wadhifa huu mara ya kwanza November 5, mwaka 2015, chini ya Rais John Magufuli.

Samia ameolewa na Hafidh Ameir mwaka 1978, na kujaaliwa watoto wanne mmoja wa kike na watatu wa kiume. Ni mtoto wake wa kike Mwanu Hafidh Ameir ndiye aliyefuata nyayo za mama yake na kuwa mwakilishi katika baraza la wawakilishi Zanzibar.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles