Uganda yaanza kupeperusha Bendera nusu mlingoti

0
659

Kampala, Uganda

Nchi ya Uganda imeanza kupeperusha benderea nusu mlingoti kufuatiwa Kifo cha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dk. John Pombe Magufuli kilichotokea Jumatano Machi 17, 2020.

Agizo hilo limetolewa Jana Machi 18, na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni na kuungana na mataifa mengine ya Jumuiya ya Afrika mashariki na Mwanamapinduzi wa Afrika kuomboleza kifo cha Rais Magufuli.

Rais Museveni alitoa Salamu za rambi rambi kabla ya kutoa agizo hilo siku ya jana katika moja ya mtandao wake wa kijamii, pia amempongeza Hayati John Pombe Magufuli kwa utendaji wake wa kazi tangu alivyoingia Madarakani Mwaka 2015.

Dkt, John Pombe Magufuli amefariki akiwa ameacha mradi mkubwa wa bomba la mafuta kutoka wilayani Hoima nchini Uganda kwenda bandari ya Tanga nchini Tanzania wa kusafirisha mafuta ya Uganda, ambapo awali viongozi wa mataifa hayo mawili walitarajiwa kusaini wiki ijayo ili kuanza rasmi ujenzi wa bomba hilo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here