25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Washtakiw 183 wafutiwa mashtaka Kagera

Na Mwandishi Wetu, Kagera

Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Biswalo Mganga, amewafutia Mashtaka jumla ya washtakiwa 183 katika magereza ya Karagwe, Bukoba, Biharamulo na Muleba mkoani Kagera.

DPP amebainisha hayo jana wakati akizungumza kwenye hafla ya ufunguzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wilaya ya Karagwe mkoani Kagera ambapo amesema kuwa mkoa huo unakabiliwa na kesi nyingi za mauaji.

Biswalo ameeleza kuwa baada ya kutembelea magereza mbalimbali na kuongea na mahabusu walioko ndani ameamua kuwafutia washtakiwa 57 toka wilaya ya Karagwe, 54 Bukoba, 48 Biharamulo na Muleba 26 huku katika ziara hiyo akikutana na badhi ya washtakiwa ambao ni wahamiaji haramu 15 waliokuwa wamekaribishwa na wazawa wa mkoa wa Kagera.

“Kimsingi kuna makosa mengi na kesi nyingi ambazo walengwa hawastahili kuwemo gerezani hivyo nimeamua kuwaachia kikubwa niwaombe viongozi wa dini muendelee kuhubiri amani,upendo ili vitamalaki kwani vitasaidia kupunguza hizi kesi,”amesema Mganga.

Aidha, Mganga amebainisha kuwa hatosita kumchukulia hatua mtu yeyote bila kujali nafasi aliyonayo kisiasa, dini au Serikali ikigundulika kuwa amejihusisha na vitendo vya Uhalifu ambapo amesisistiza suala la amani ni jukumu la kila mtu hivyo wanawajibika kuitunza kwa kuepuka kufanya makosa ya jinai.

Kwa upande wake Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Kagera, Ntemi Kilekamajenga amesema mkoa wa Kagera unaongoza kwa kuwa na kesi nyingi za mauaji ambapo amewaomba viongozi wa dini kuendelea kuhubiri amani ili kupunguza vitendo vya uhalifu.

Jaji Ntemi amesema kesi nyingi zinaweza kuishi kwa njia ya usuluhishi nje ya mahakama hivyo kuipunguzia serikali gharama za uendeshaji wa kesi.

Aidha, Jaji Ntemi amesema Mkoa wa Kagera kesi ambazo zipo katika hatua ya kusikilizwa zinakaribia kuvuka 450 hivyo mkoa wa Kagera unaweza kuwa wa pili au watatu kwa Tanzania kuwa na kesi nyingi za mauaji.

Askofu wa Jimbo Katoliki la Kayanga, Almachius Rweyongeza amebainisha kuwa kufunguliwa kwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka katika wilaya ya Karagwe kutasaidia wananchi kupata haki kwa wakati sambamba na kuwakumbusha viongozi wenzake wa dini kutimiza wajibu wao wa kuhubiri upendo na amani kwa mujibu wa maandiko matakatifu.

Mwakilishi wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) Mkoa wa Kagera Liberatha Bamporiki ameeleza kufunguliwa kwa Ofisi hiyo ya Mashtaka katika wilaya ya Karagwe kutapunguza gharama na muda mwingi waliokuwa wakiutumia kwenda Manispaa ya Bukoba kufautilia kesi zao hali itakyoaaidia kasi ya mashauri kuongezeka na kusaidia kukamilika kwa wakati.

Nao baadhi ya wakazi wa Karagwe akiwemo, Clemence Isherenguzi na Selestine John wamesema kuwa kufunguliwa kwa ofisi hiyo ni ukombozi kwao kutokana na awali walikuwa wakitumia gharama kubwa kusafiri toka Karagwe kwenda Manispaa ya Bukoba umbali kufauta huduma za mashtaka ambapo kwa sasa uwepo wa ofisi hiyo utasaidia kupunguza mzigo wa gharama kwa wananchi wa wilaya ya Karagwe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles