26.7 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Mgombea Urais TPC ataja vipaumbele

Na Victoria Godfrey, Dar es Salaam

Mgombea wa nafasi ya Urais wa Kamati ya Paralimpiki Tanzania ( TPC), Tuma Dandi, ametaja vipaumbele atakavyotekelezwa baada ya kupata ridhaa ya kuingia madarakani.

TPC inatarajia kufanya Uchaguzi Mkuu Januari 23, mwaka huu, kwenye Ukumbi wa Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Dandi ameiambia MtanzaniaDigital kuwa vipaumbele hivyo ni pamoja na kuifanya michezo ya watu wenye ulemavu kuwatangaza wahusika na kupunguza unyanyapaa dhidi yao.

Dandi amesema baada ya kuunda vyama sasa kazi ni kuviunganisha na wadau ili wanamichezo wao waweze kuhimili ushindani .

Pia amesema kipaumbele kingine ni kukuza vipaji vichanga kwa sababu wachezaji waliopo wengi ni wazee na pia wanacheza kwa ridhaa.

“Hivi baadhi ya vipaumbele ambavyo tutavitekeleza baada ya kupata ridhaa ya uongozi tukiwa na nia ya kuhakikisha maendeleo ya michezo yanapatikana kwa watu wenye Ulemavu,” amesema Dandi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles