25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Wakulima Kagera wapokea mbegu za Michikichi

Na Renatha Kipaka, Bukoba

Wakala wa Mbegu nchini, ASA imetoa miche 8,000 ya michikichiki kwa Mkoa wa Kagera ikiwa ni uanzishaji wa kilimo hicho na uzalishaji wa mafuta ya Mawese mkoani humo.

Itakumbukwa kuwa zoezi hilo lilianzishwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mwaka 2018​ kama zao la kimkakati lengo likiwa ni kusaidia kutoingizwa kwa mafuta ya kula nchini.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mtendaji Mkuu wa ASA, Sophia Kashenye​ wakati akielezea umuhimu wa kuangalia fursa na matumizi ya zao hilo kwa ajiri ya kuwa na ongezeko la mafuta na usalama wa chakula.

Kashenye amesema, kumekuwa na upungufu wa chakula kwa asilimia 2 .9 ikilinganishwa na ongezeko la watu asilimia 3.1.

Nassor Mtengaliki ni msimamizi wa kikundi cha uchukuaji mbegu ambaye amesema kuwa miche hiyo imeonekana kupendwa na wakulima licha ya kuwa na mazoea ya kilimo cha mibuni na migomba.

Mtengaliki amesema zao hilo linafaida nyingi na sio mafuta pekee bali hutengeneza nyingine kama bidhaa za sabuni kama sehemu za ujasiriamali wa kuwa na bidhaa mbalimbali zitokanazo na mafuta ya mawese.

Rei Renatusi mkazi wa mtaa wa Kashai amesema ili kunufaika na kufanikiwa na kilimo hicho lazima wahusika wa kilimo wapewe elimu itakayosaidia kulima na kutunza miche hiyo.

“Tumezoea kulima mikahawa, migomba viazi na vanila hili zao ni geni hapa kwetu tulienda na inawezekana kulima endapo tu tutapewa elimu ya kulima,” anasema Renatus.

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Isaya Tendega amesema, Mkoa huo una hali ya hewa nzuri hivyo uwezekano wa kufanikisha uzalishaji wa kilimo hicho ni mkubwa ikilinganishwa na watafiti wanavyoeleza.

Amesema ili kuongeza kipato cha mkoa na mtu mmoja mmoja lazima mkulima ajihusishe na kilimo mbalimbali ikiwemo michikichi hiyo kama jinsi ilivyo mkoa wa Kigoma unavyozalisha zao hilo.

Aidha, amesema kwa mujibu wa watafiti wa kilimo​ miche hiyo​ hukomaa baada ya miaka mitatu kwani ni miche bora ya muda mfupi kuanza kupata mavuno.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles