28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Uingereza yapiga marufuku abiria kutoka Tanzania, DRC

London, Uingereza

Serikali ya Uingereza imepiga marufuku abiria kutoka Tanzania na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kuzuia maambukizi ya aina mpya ya virusi vya corona.

Marufuku hiyo imetolewa jana Januari 21, na Waziri wa Uchukuzi wa Uingereza, Grant Shapps kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter.

“Ili kusaidia kuzuia kuenea kwa aina ya COVID-19 iliyogundulika Afrika Kusini, tunapiga marufuku abiria wote wanaoingia kutoka Tanzania na DRC kuanzia saa 10 alfajiri kesho(leo Ijumaa),” ameandika Grant Shapps, Waziri wa uchukuzi nchini Uingereza kupitia mtandao wake wa Twitter Alhamisi usiku.

Zuio hilo linaanza kwa wasafiri wote waliotoka ama kupita nchini Tanzania na DRC ndani ya siku 10 zilizopita. Hata hivyo, raia wa Uingereza na Ireland na raia kutoka mataifa mengine ambao wenye vibali vya ukaazi wataruhusiwa kuingia ila watatakiwa kujitenga nyumbani pamoja na familia zao kwa siku 10 baada ya kuwasili.

Tanzana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zimeongezwa kwenye orodha ya Uingereza ya nchi zilizopigiwa marufuku ya wasafiri wake kuingia nchini humo kama hatua za kudhibiti maambukizo ya aina mpya ya virusi vya Corona vilivyogunduliwa nchini Afrika Kusini.

Mapema mwezi huu mataifa mengine 11 ya Afrika yalipigwa marufuku kama hiyo. Mataifa hayo ni; Namibia, Zimbabwe, Botswana, Eswatini, Zambia, Malawi, Lesotho, Msumbiji na Angola – visiwa vya Ushelisheli na Mauritius. Uingereza ilipiga marufuku abiria kutoka Afrika Kusini Desemba 24.

Uingereza ni miongoni mwa mataifa ambayo yanakabiliana na janga la virusi vya corona kwa kiwango kikubwa na uchumi wake ukiwa umeyumba kutokana na wimbi la kwanza la virusi mambukizi ya corona.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles