28 C
Dar es Salaam
Friday, February 23, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania Prisons kuingia kambini Jumapili

Na Victoria Godfrey, Dar es Salaam

Kikosi cha Tanzania Prisons kinatarajia kuanza mazoezi Jumapili hii kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL).

Katibu Mkuu wa Prisons, Ajabu Kifukwe, ameiambia MtanzaniaDigital kuwa wachezaji wote wanatarajia kuripoti kesho kambini mkoani Rukwa.

Amesema wachezaji hao watajumuishwa na wale waliosajiliwa kwenye dirisha dogo kwa ajili ya kuongeza nguvu katika kikosi hicho.

“Baada ya mapumziko mafupi sasa wachezaji wanatarajia kurejea kesho kambini kuanza mazoezi rasmi kwa mzunguko wa pili wa ligi,” amesema Kifukwe.

Kifukwe amesema malengo yao ni kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye mzunguko wa pili ili wajiweka katika nafasi mzuri msimu ujao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles