24.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 27, 2024

Contact us: [email protected]

Marekani kuanza tena kufadhili WHO

Washington, Marekani

Marekani itaanza tena kufadhili Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) na kujiunga katika ushirika unaolenga kugawanya chanjo ya virusi vya corona kote ulimwenguni huku, Rais Joe Biden akitilia mkazo sheria za kuzuia maambukizi ya virusi hivyo.

Hatua hiyo iliyotangazwa jana Januari 21, na mshauri mkuu wa rais Joe Biden kuhusiana na janga la virusi vya corona, Dkt Anthony Fauci, inafufua upya uungwaji mkono wa shirika ambalo uongozi wa Trump ulijitenga nalo.

Kujitolea haraka kwa Dk. Fauci kwa WHO ambalo mikakati yake ya kushugulikia janga la virusi vya corona ilikosolewa na wengi, lakini zaidi na utawala wa Trump, kunaashiria mabadiliko katika hatua ya ushirikiano zaidi katika kukabiliana na janga hilo.

Dk. Fauci ameongeza kusema kwamba anafurahia kutangaza kwamba Marekani itabaki kuwa mwanachama wa WHO na kwamba rais Biden alitia saini barua zinazoondoa tangazo la awali la utawala wa Trump kujiondoa katika shirika hilo.

Hili ni tangazo la kwanza la umma la Afisa wa serikali ya Biden kwa hadhira ya kimataifa na ishara ya kipaombele ambacho rais huyo mpya ametoa katika vita dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 nchini humo pamoja na washirika wa kimataifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles