Na Jeremia Ernest
Washiriki wa Miss Tanga wametembelea hospitali ya Bombo iliyopo jijini humo katika wodi ya watoto kwa ajili ya kugawa baadhi ya mahitaji na kuzungumza na wagonjwa.
Baadhi ya mahitaji waliyoenda nayo ni maziwa, sabuni, dawa za mswaki, miswaki na mafuta ya kupaka.
Akizungumza na Bingwa leo Julai 4, muaandaji wa shindano hilo, muigizaji Chuchu Hans amesema tukio hilo hii ni ishara ya kuwa mshindi atakayepatikana atatumikia jamii yake.
” Urembo una maana nyingi ikiwamo na kuijali jamii na kuitumikia kwa kuchangia maendeleo mbalimbali pamoja na kuwajali wenye mahitaji maalum ili wasikate tamaa kwa yale wanayopitia,” amesema Chuchu.
Kinyanga’nyiro hicho kinatarajiwa kufanyika Julai 6, Tanga hotel na kupambwa na mastaa mbalimbali akiwemo Johari, Dully Sykes, Duma na Gabozigamba huku kiiingilio kikiwa 50,000, 30,000 na 10,000.