28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

WAPINZANI DRC WATISHIA KUANDAMANA

 

KINSHASA, Congo DRC


Chama Kikuu cha upinzani nchini hapa, MCL, kimetishia kufanya maandamano makubwa  ya  kuupinga uchaguzi mkuu, baada ya Mahakama ya Katiba  kusema mgombea wake, Jean-Pierre Bemba, hana vigezo vya kugombea nafasi ya urais.

Hatua ya chama hicho imekuja baada ya jina la  Bemba kuondolewa  kwenye orodha ya wagombea nafasi ya urais,  baada ya kukosekana ushahidi wa kutosha na mahakama hiyo kukosa imani na upande wa ushahidi  uliotolewa katika Mahakama ya Kimataifa inayoshughulikia makosa  ya Uhalifu wa Kivita (ICC).

Baada ya kufanyika vikao vya ndani, chama hicho cha MCL kimetangaza rasmi kuwa kitatangaza baadaye tarehe rasmi ya maandamano hayo, ili kupinga uamuzi wa Mahakama hiyo ya Katiba  kuondoa jina la mgombea wake  katika uchaguzi mkuu ujao unaotarajiwa kufanyika miezi minne ijayo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mapema jana na chama hicho, kimeuchukulia uamuzi ya mahakama hiyo ya Katiba kama ya ovyo na unaweza kuiingiza nchi hii katika machafuko.

Katika taarifa ya chama cha Bemba, kimekitupia mzigo wa lawama tume ya uchaguzi pamoja na mahakama nchini humo kwa kuwa imejaa siasa jambo ambalo Serikali imelipinga kwa nguvu zote.

Inaelezwa kuwa kiongozi huyo mwenye ushawishi mkubwa nchini hapa ambaye alikuwa mjini Brussels nchini Ubelgiji, aliyerejea mjini hapa mwezi huu, lakini kurejea kwake tena nchini humo kumeahirishwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles