31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

MWANAFUNZI AJIUA AKILAZIMISHWA KUKIRI KUMPA MIMBA MWENZAKE

 

Na SAFINA SARWATT, KILIMANJARO


Mwanafunzi  wa Kidato cha nne, Emmanuel Tarimo (18) wa Shule ya Sekondari Rau iliyopo  wilayani Moshi, mkoani Kilimanjaro amejinyonga hadi kufa baada ya kulazishimishwa na mwalimu wake kukiri kumpa ujauzito wanafunzi wa kitado cha kwanza ujauzito.

Mwanafunzi huyo inadaiwa kabla ya kujinyonga alihojiwa na timu ya walimu wa shule hiyo kwa zaidi ya saa 12 huku wakimtaka akiri kwamba alimpa mimba mwanafunzi mwezake.

Inadaiwa mwanafunzi huyo kabla ya kifo chache aliwekwa kikaangoni na walimu wake waliomshikiniza kukiri kutenda kosa hilo lakini baadaye ilibainika msichana aliyedaiwa kuwa na mimba hakuwa nayo.

“Walikuwa wamemfungia ndani ya ofisi na kumtaka akiri kwamba mimba ni ya kwake huku wakimtishia, tunaomba serikali ilifuatilie tukio hilo ili haki itendeke,” walidai baadhi ya wanafunzi waliozungumza na MTANZANIA.

Dada wa marehemu, Tedy Maro alisema ni jambo lisiloingia akilini mdogo wake kuchukua uamuzi mgumu wa kujinyonga kama asingetishiwa maisha na walimu.

“Ndugu yetu alipewa vitisho na walimu ndiyo maana alichukua hatua ya kujiua, tunaomba serikali ichunguze hili tukio kwa sababu limetupa fedheha kubwa sana familia.

“Hata kama alifanya kosa ilitakiwa wazazi wapewe taarifa ili watafute namna ya kulishughulikia tatizo hilo,” alisema Maro.

Babu wa Mwanafunzi huyo, Jerome Maro aliiomba serikali iwafuatilie madai ya vitisho vilivyotolewa na walimu.

Erick Mshanga, ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha nne wa shule hiyo, alisema tukio la mwanafunzi mwenzake kujinyonga limewaumiza kwa sababu hata kama alikuwa ametingwa na mambo mengi angewashirikisha kuliko kujinyonga.

Akijibu tuhuma hizo, Mkuu wa shule hiyo, Nyoni Njinjinji alikiri kuhojiwa kwa wanafunzi huyo baada ya kudaiwa kujihusisha kimapenzi  na mwanafunzi mwenzake wa kidato cha kwanza.

“Marehemu alidaiwa kujihusisha kimapenzi na mwanafunzi wa kidato cha kwanza na baada ya tuhuma hizo walihojiwa na walimu wa nidhamu,” alisema Njinjinji.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Hamis Issah alithibitisha kutokea kwa kifo cha mwanafunzi huyo kwa maelezo kuwa alijinyonga akiwa sebuleni kwao kwa kutumia mkanda wa suruali yake.

Kamanda Issah alisema tukio hilo limetokea Septemba 4, mwaka huu majira ya saa tano usiku baada ya mwanafunzi huyo kukutwa akiwa amejiningiza nyumbani kwao akiwa amekwishakufa.

“Baada ya kufuatilia walibaini kwamba kijana huyo siku tatu kabla ya kifo chake alituhumiwa kujihusisha kimapenzi na wasichana zaidi ya mmoja na kwamba kitendo hicho cha kuitwa na walimu na kumhoji kilimfedhehesha, mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro, Mawenzi,” alisema.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles