26.1 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Wapenzi wafunga ndoa maeneo hatarishi

SI jambo linaloweza kufikiriwa na kila mtu kulitenda wakati wa siku maalumu ya ndoto yake.

Jambo gani? Lile ambalo linaweza kupoteza uhai wako katika siku hiyo ya ndoto yako. Ni siku gani? Miongoni mwao ni harusi.

Ni kwa vile kwa wengine ni tukio la mara moja au mbili kwa maisha yao achilia mbali wale wanaooa na kuacha au kuachika mara kwa mara, ambao tukio hilo hupoteza msisimko.

Lakini baadhi ya wapenzi nchini China huchagua kusherehekea na hata kufunga ndoa zao kwenye maeneo hatari.

Miongoni mwa maeneo hayo ni madaraja ya vioo, madaraja yanayoning’inia hewani na au katika majabali marefu na hatari duniani.

Miongoni mwa matukio yaliyofuatiliwa sana ya harusi aina hizo ni ya bwana na bibi harusi waliooana wakati wa Siku ya Wapendanayo ya Kichina inayoadhimishwa Agosti 9.

Walioana katika Daraja la Shiniuzhai lililopo mji wa Pingjiang jimbo la Hunan, kwa mujibu wa Shirika la Habari la China (CNS).

Licha ya kuelea angani yapata futi 590 kutoka usawa wa ardhi , wenzi hao waliweza kuonyesha tabasamu lao pana walipokuwa wakipigwa picha za harusi yao.

Madaraja ya vioo yamekuwa maarufu sana nchini China hivi karibuni. Wanandoa wengine walipigwa picha wakining’inia kwenye jabali refu  lililopo Milima Chaya katikati mwa China.

Na wengine wakiwa wamepozi katika bendera zinazoelea angani, ambazo zinahitaji watu majasiri kufanya hivyo, vinginevyo usiombe!

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles