28 C
Dar es Salaam
Friday, February 23, 2024

Contact us: [email protected]

Wanyama aimwagia sifa Southampton

Celtic v Barcelona - UEFA Champions LeagueLONDON, ENGLAND

KIUNGO wa timu ya Taifa ya Kenya na klabu ya Southampton ya nchini England, Victor Wanyama, ameimwagia sifa klabu yake ya Southampton kwa ushirikiano ambao waliuonesha kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Arsenal ambapo Southampton iliibuka na ushindi wa mabao 4-0 mwishoni mwa wiki iliyopita.

Mtandao wa Supersport umeripoti kwamba, Wanyama amekuwa na furaha kubwa baada ya kuisaidia timu yake Southampton kuweza kuibuka na ushindi katika Sikukuu ya ‘Boxing Day’ kwa kuichapa Arsenal.

Mchezaji huyo ambaye awali alitarajiwa kutua katika klabu hiyo ya Emirates, alionesha kiwango cha hali ya juu katika mchezo huo wa mwishoni mwa wiki iliyopita.

“Nimekuwa na furaha kubwa tangu tulipopata ushindi dhidi ya Arsenal, hii ilitokana na ushirikiano uliopo kwa wachezaji na viongozi wake. Hii ilikuwa ni siku ya kukumbukwa kwa upande wangu kwa kuwa ilikuwa ni siku ya sikukuu ya zawadi.

“Kilichobaki kwa sasa ni kuangalia michezo mingine ambayo inakuja mbele yetu kwa kuwa ligi bado inaendelea na kuna ushindani mkubwa sana,” alisema Wanyama.

Southampton ilicheza michezo mitano ya nyuma bila ya kupata ushindi kabla ya mchezo dhidi ya Arsenal, lakini klabu hiyo imejipanga kuutumia mfumo ambao waliutumia dhidi ya Arsenal ili kuweza kuibuka na ushindi katika michezo ijayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles