24.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 11, 2024

Contact us: [email protected]

Mchezaji auawa kwa risasi El Salvador

hi-res-a722137262ef00900639118f5faf3117_crop_northSAN SALVADOR, EL SALVADOR

NYOTA wa zamani wa klabu ya New York Red Bull ya nchini Marekani na timu ya taifa ya El Salvador, Alfredo Pacheco, ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana nchini humo.

Beki huyo wa pembeni ambaye alikuwa na umri wa miaka 33, alishambuliwa kwa risasi katika kituo cha mafuta katika mji wa Santa Ana, kilomita 76 Magharibi mwa mji mkuu wa San Salvador.

Polisi nchini humo wamesema watu wengine wawili walijeruhiwa kwenye shambulio hilo lakini polisi bado wanachunguza chanzo cha tukio hilo.

Mlinzi huyo aliyechezea El Salvador mechi nyingi zaidi za kimataifa, lakini alifungiwa kuitumikia timu hiyo maisha kutokana na hatia ya kupanga matokeo 2013.

Pacheco na wachezaji wengine 13 walipatikana na hatia ya pokea hongo timu hiyo ishindwe baadhi ya michezo kati ya mwaka 2010-13.

El Salvador, Taifa ndogo lililoko Amerika ya Kati, ni moja ya mataifa yenye viwango vya juu zaidi vya mauaji.

Mapema mwezi huu, mchezaji wa timu ya taifa ya Honduras, Arnold Peralta, 26, aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa likizo nchini humo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles