31.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 28, 2023

Contact us: [email protected]

Hiddink aipa ubingwa Leicester City

01_23131636_5c3c07_2615269aLONDON, ENGLAND

KOCHA mpya wa klabu ya Chelsea, Guus Hiddink, amedai kwamba hashangazwi na uwezo wa Leicester City msimu huu na kuna uwezekano mkubwa wa kuendelea kufanya vizuri na kuchukua ubingwa.

Klabu hiyo imekuwa ikiongoza katika msimamo wa Ligi Kuu nchini England kabla ya mchezo wa jana, hivyo kocha huyo ambaye amechukua nafasi ya Jose Mourinho katika klabu ya Chelsea, Hiddink, amesema Leicester City wana nafasi kubwa ya kuendelea kufanya vizuri msimu huu.

“Sishangazwi na mafanikio ya Leicester City katika michuano ya Ligi Kuu nchini England, siku zote ligi hiyo inakuwa haitabiriki chochote kinaweza kutokea na ninaamini klabu hiyo itaendelea kufanya vizuri.

“Japokuwa klabu hiyo ilipoteza mchezo wake dhidi ya Liverpool mwishoni mwa wiki iliyopita, lakini bado wana nafasi kubwa ya kuendelea kuongoza katika ligi hiyo,” alisema Hiddink.

Mbali na Hiddink kuipa nafasi klabu hiyo, lakini amesema kuwa kuna klabu nyingine ambazo zinaweza kushangaza watu msimu huu ambazo ni Crystal Palace na Watford.

“Kuna timu ambazo zinaonekana kujiandaa vizuri, lakini endapo zinakutana na klabu kama Leicester City, Watford na Crystal Palace kuna uwezekano mkubwa wa kufungwa kwa kuwa timu hizi kwa sasa zinafanya vizuri,” aliongeza Hiddink.

Chelsea ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini England, wamekuwa na wakati mgumu msimu huu kutokana na kupoteza michezo mingi ambapo ilichangia kumfukuza kocha wake, Mourinho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles