25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Wanufaika wa TASAF Iramba wapewa somo

Na Seif Takaza, Iramba

MKUU wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Suleiman Mwenda, amewahimiza wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya masikini (TASAF) wilayani hapa, kutumia fedha walizopata kununulia mbegu bora na pembejeo kwa ajili ya maandalizi ya kilimo msimu huu.

Akizungumza na wanufaika wa mpango huo  katika vijiji vya Kitukutu na Kyengege, hivi karibuni, Mwenda amesema Serikali ya Tanzania  inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan  imetoa fedha nyingi kwa shughuli za  maendeleo katika nyanja zote,  hivyo kila mmoja awajibike katika kufanya kazi za uzalishaji mali ili kila mwananchi aondokane na umaskini .

‘’Ndugu zangu wanufaika na mradi huu wa kunusuru kaya maskini  nawaombeni mtumie fedha hizi mlizopata kwa ajili ya kununulia mbegu bora na pembejeo za kilimo  kwa ajili ya  kilimo msimu huu, hivyo kila mmoja wenu  anatakiwa kujipanga vizuri katika matumizi mazuri  ya fedha hizo,” Amesisitiza Mwenda.

Amewataka wananchi wa wilaya hiyo walime mazao ya chakula na  biashara ili kila kaya kuwa na chakula cha kutosha.

‘’Serikali yenu imetoa ruzuku kwa ajili ya zao la alizeti hivyo mnapaswa kujiandaa vizuri na kilimo msimu huu wa kilimo ili muweze kulima alizeti kitaalam na kwa kutumia mbegu bora tuweze kujitosheleza kwa mafuta ya kupikia,’’ amesema.

Kwa upande wake Mratibu wa TASAF wa  Halmashauri hiyo, Frida Lwanji  amesema mpango wa kunusuru kaya maskini  unaendelea kutekelezwa kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi .

‘’Mpango huu  wa kunusuru kaya masikini umesaidia   kuziwezesha  kaya hizo  kupata huduma za kijamii kama vile  chakula na  mavazi na  kuanzisha miradi ambayo  imewaongezea kipato. 

“Katika miradi hiyo baadhi ya kaya zimepata  maendeleo  ambapo wengine wamefuga kuku, mbuzi,nguruwe  na wengine wamejenga nyumba kwa kutumia fedha za ruzuku wanazopata.

 ‘’Wilaya ya Iramba ni miongoni mwa wilaya ambazo zinazotekeleza mradi wa kunusuru kaya maskini na tunatekeleza katika vijiji 51,  na  jumla ya kaya 5164  zinanufaika na mpango huo ambapo ni sawa na asilimimia 70 lakini pia tunatarajia kunufaisha walengwa wa wa mradi huu kwa vijiji 27 ni sawa na asilimia 30 malipo haya tunayofanya sasa ni kwa miezi Mei na Juni 2021,” amesema Lwanji

Naye Ofisa ufuatiliaji wa mpango wa TASAF,Andrew Nguni amesema jukumu lake ni kufuatilia miradi kwa wanufaika wa kaya masikini kuwa katika ubora unaotakiwa

‘’ Miradi ninayofuatilia ni pamoja  na ajira ya muda mfupi, uhaulishaji wa fedha  mradi wa timiza malengo kwa wasichana balehe waliopo mashuleni na nje ya mfumo wa shule  na kuweka akiba na kuwekeza’’amefafanua Nguni .

Naye mnufaika wa kijiji cha Kitukutu,  Rozi Donki ameishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Samia kwa kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo kama vile ujenzi wa zahanati , vituo vya afya ,ujenzi wa madarasa miradi ya maji, barabara na maendeleo ya jamii kwa ujumla.

Edson Selemani wa kijiji cha Kyengege alimhakikishia Mkuu wa Wilaya kuwa   wanamuunga mkono Rais Samia katika shughuli za maendeleo na kushukuru kwa   kuwapelekea mbegu bora ya alizeti na pembejeo nan kumuomba Mkuu wa Wilaya zipekwe mapema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles