27 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi Muleba watakiwa kushirikiana kuleta maendeleo

Renatha Kipaka Muleba

Wananchi na Viongozi wa kijiji cha Kangaza wilayani Muleba mkoani Kagera wameshauriwa kuhakikisha wanakuwa na ushirikiano wa pamoja ili kuleta maendeleo katika kijiji chao.

Ushauri huo umetolewa leo Jumatano Novemba 3, katika no wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Kangaza, kata ya Nyakabango wilaya ya Muleba kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zilizopo katika kijiji hicho.

Hata hivyo, akizungumza katika mkutano huo Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Toba Nguvila amewasisitiza viongozi wa eneo hilo kuacha malumbano na badala yake kuelekeza nguvu zao katika shughuli za maendeleo kwani kuishi kwa malumbano kunachelewesha maendeleo katika maeneo yao na kuwahimiza kuwepo na mahusiano mwema baina yao na Serikali.

Nguvila amewasisitiza wananchi wa eneo hilo kutoshiriki katika shughuli za uvuvi haramu kwa sababu uvuvi haramu unaweza kupelekea kupungua kwa samaki, kuharibu mazalia ya samaki na kukosekana kwa vitoweo ho katika Ziwa Victoria.

“Eneo hili la mwambao wa ziwa kuanzia Nyakabango mpaka Mganza ni lamazalia ya samaki, ipo tabia ya kutumia nyavu zisizokubalika kisheria sasa hatutamvumilia mtu atakayevunja utaratibu,”amesema Nguvila na kuongeza kuwa;

“Kuna kokoro moja linaweza kuvua hata tani nzima ambapo samaki wanaovuliwa na ni wadogo ambao hata huwezi kuwapeleka kiwandani wala kuuza sokoni, lakini kama samaki wale wangeachwa hata kwa kipindi cha miezi sita tu wangeweza kuwa wakubwa kiasi cha kuwa na kilo 100 kwa hiyo acheni uvuvi haramu kwa ajili ya kulinda uvuvi endelevu,”amesema Nguvila.

Aidha, amewasisitiza wananchi wa eneo hilo kuhamasika na shughuli za kilimo cha mazao ya chakula na biashara kama kilimo cha kahawa, maharage, mpunga, pamba, mahindi pamoja migomba hasa kwa kuongeza ukubwa wa mashamba.

Ameongza kuwa wananchi na bima za afya kwa kujiunga na Bima ya Afya ya Jamii iliyoboreshwa (CHF) inayotolewa kwa gharama ya Sh 30,000 kwa familia ya baba na mama na watoto wanne ili kuepukana na tabu ya kwenda kwenye vituo vya afya kupata huduma ya tiba kwa gharama kubwa na wakati mwingine wakiwa hawana fedha ya matibabu.

Aidha, amezungumzia suala la elimu na kuwasisitiza wananchi kuhamasika kuchangia vyakula vitakavyowezesha watoto kupata chakula wanapokuwa shuleni ili watoto waweze kuongeza ufaulu kwani watoto wakipewa chakula shuleni itawasaidia kusoma kwa utulivu.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Muleba, Stewart Mtondwa amewaonya na kuwasisitiza wananchi kuwa makini sana kwa kuhakikisha hawawaruhusu watoto wao kuogelea kwenye mwambao wa ziwa kuepuka kujeruhiwa na mamba baada ya kutokea kwa tukio la mtoto kujeruhiwa na mamba katika kijiji hicho.

Amesisitiza mtendaji wa kijiji kwa kushirikiana na Mwenyekiti kuhakikisha wanaitisha vikao na mikutano na kuwasomea wananchi wa eneo hilo mapato na matumizi kila baada ya miezi mitatu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles